Music

banner image

Header Ads

Header ADS

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

SIMULIZI | Facebook Love sehemu ya Tatu

Facebook Love 
Simulizi
SIMULIZI: FACEBOOK LOVEE 03 Natasha ana mwanaume wake, jamaa mmoja mwenye mkwanja wa maana, na anampenda sana, Nilichomwambia ni kwamba jamaa anataka kuonana naye amwambie ukweli tu macho kwa macho, wengine wamezaliwa na bahati zao hivyo anaweza kukubaliwa, Kwanza Rose akakataa, lakini baada ya kumchombezachombeza, akakubali akanielekeza anapoishi Natasha, tukaagana. Maneno yake yakanichanganya sana, nikawasiliana na Natasha, jinsi tulivyokuwa tukichati, alivyokuwa akinipa ahadi za kunipenda milele, ilikuwa ngumu kuamini kama kweli msichana aliyemzungumzia Rose alikuwa Natasha huyuhuyu nayemjua mimi Nilichokifanya ni kuondoka nyumbani siku inayofuata na kwenda mtaani kwao, alikuwa akiishi Sinza Vatican, nilipofika huko mpaka nyumba ali moja kali limepaki nje kwao, nililiangalia, lilikuwa la kifahari sana, ghafla geti likafunguliwa, nikajificha, akatoka Natasha, mlango wa gari ukafunguliwa, akatoka Jamaa, wakakumbatiana na kisha kubadilishana mate, iliniuma sana nikapiga picha harakaharaka na kuondoka zangu Nilipofika nyumbani , sikuacha kuchati naye, nilimpenda kwa moyo mmoja, sikuamini kama yule niliyemuona alikuwa yeye wakati mwingine nikahisi kama nilimfananisha hivyo kumuuliza kama alikuwa na pacha wake, akasema hapana, yupo peke yake na hawajazaliwa mapacha akut: kuwa akiishi, na gari Sikutaka kumwambia nilichokiona, nilijifanya kumsisitizia ni pafahamu kwao lakini bado alinizingua pasipo kujua kwamba ninapafahamu Hiyo haikuwa mwisho, mara kwa mara nilikuwa namfumania mazingira ya kwao, tena akiwa na mwanaume huyohuyog walikuwa kwenye mapenzi ya dhati. Siku zikakatika, kuna siku nilimwambia kwamba nataka kuonana naye, kwelf tukaonana, ilikuwa katika hoteli ya Flawless iliyokuwa Mikocheni, hapo, nilimwambia ukweli kuhusu hisia zangu kwake, nilitaka ajue ni jinsi gani nilikuwa nikimpenda, alitabasamug akafurahi sana, nikamuuliza swali moja, alikuwa tayari kuolewa mimi? na #ITAENDELEA
SIMULIZI | Facebook Love sehemu ya Tatu SIMULIZI | Facebook Love sehemu ya Tatu Reviewed by Siabi World on July 22, 2019 Rating: 5

No comments:

title-header