Music

banner image

Header Ads

Header ADS

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

STORY | FACEBOOK LOVE Sehemu ya kwanza no.1

Facebook Love no.1

 SIMULIZI FACEBOOK LOVEE 01 Mara ya kwanza nilikutana na Natasha humu Facebook. Nikamchombeza kwa maneno matamu, akatokea kunifagilia, tukachati na kuchati, akaniambia anaona wivu nikiLIKE picha za wasichana wengine, hivyo nikaacha, Wakati ukaribu ukiendelea, nikamuomba namba ya simug harakaharaka akanipa, siku hiyohiyo nikampigia simu usiku, tukaongea sana, nikamchekesha kwa vijistori vya hapa na pale akafurahi sana. Sikuwa nimetongoza japokuwa alijua ninampenda sana, siku nilipoamua kufanya hivyo akanichomolea, akaniambia ananichukulia mimi kama kaka, na yeye anataka nimuone kama dada, sikuwa na jinsi nikakubaliana naye Baada ya wiki moja, nikampigia simu, nikamwambia "Dada nataka unishauri, kuna msichana anatamani sana kuwa nami je nimkubalie?" akaniambia nikatae lakini pia akanisisitiza nionane naye siku inayofuata, nikakubaliana naye. Kweli siku hiyo ilipofika, nikaulamba, nikapendeza sana, nikaondoka na kwenda kuonana naye Msasani, ile kukutana, akanisogelea na kuunikumbatia, alinukia vizuri sana, tukazungumza na kwenda sehemu kula, huko, akaniambia kwamba ANANIPENDA Kwanza sikuamini, nilimwambia inakuwaje dada kumpenda kaka? Akaniambia kwamba alishindwa kuvumilia, wakati nimekaa huku nikijiuliza, akanisogelea, akanipiga busu murua mdomoni kweli nikahisi ulaini wa lipsi zake, harufu nzuri ya manukato, hakika ilinipagawisha, Siku hiyo ndiyo tukaanza uhusiano wa kimapenzi, kumbuka hatukuwahi kufanya mapenzi. Siku hiyohiyo, akabadilisha picha Whatsapp na kuniweka mimîg na mimi nikamuweka huku pikiandika status My Lovie, Nothing will Do Us Apart, Mapenzi yakawa matamu Sana, tuliwasiliana kila siku na kila saa, baada ya wiki nne akaniambia kwamba anataka kuja kunitembelea, nikakubali, hivyo nikamualika, Kweli akaja, kilichofuata, nadhani wengi mnakijua, tukaridhika sana na hivyo kuliongeza penzi letu kutoka moja mpaka mbilie #ITAENDELEA
STORY | FACEBOOK LOVE Sehemu ya kwanza no.1 STORY | FACEBOOK LOVE Sehemu ya kwanza no.1 Reviewed by Siabi World on July 20, 2019 Rating: 5

No comments:

title-header