Music

banner image

Header Ads

Header ADS

Custom Widget

3/Business/post-per-tag

Kwanini Watu Huachana Katika Mapenzi?



Kwanini watu wanaachana katika mapenzi? Kwanini watu ambao uliwaona kama wanapendana, walitongozana wakaingia kwenye mahusiano na hata kuingia kwenye ndoa huachana na kila mmoja kuchukua ustaarabu wake. Kuna sababu nyingi za watu kuachana na hizi hutofautiana kati ya mwanamke na mwanaume, wakati nitajadili sababu mbalimbali katika makala nyingine katika makala hii nitajadili sababu za jumla za watu kuachana.
Kuna sababu kuu nne za jumla za watu kuachana, sababu ya kwanza ni kua hakukua na mapenzi kabisa, sababu ya pili ni mmoja kushindwa kuvumilia, sababu ya tatu ni kutokea kwa mtu mpya na sababu ya nne ni kuzoeana. Nimuhimu ukazifahamu sbaabu hizi kwani wakati mwingine unaweza kujilaumu na kujiona kam auna mikosi kwa kuachika kumbe sababu haikua wewe.
 (1) Hakukua Na Mapenzi; Hii ni sababu ya kwanza, kitenganishi kikubwa cha watu, kitu ambacho huwafanya watu kuvumiliana mapungufu yao ni mapenzi. Kama hakuna mapenzi kati ya wili basi nirahisi kuachana kwani ni ngumu kuvumiliana.
Sasa inawezekana kuwa, mmoja wenu aliingia kwenye mahusiano kwasbaau binafsi, labda hakumpenda mhusika lakini alikua akimhitaji kwa wakati huo. Alikua na mambo yake, labda alitaka ngono, labda pesa, labda alitaka kumsahau mtu wake wa awali.
Kwa maana hiyo kwamba akishamaliza au akishapata kile ambacho kilimfanya kuingia katika mahusiano basi anakua ameshamaliza na humucha mwingine. Inawezekana wote mlikua hampendani au ni mmoja.
Kama wote mlikua hampendani basi si shida sana kwani hakuna atakayeumia lakini kamammoja alikua anapenda na mwingine alikua na sababu binafsi ambazo si mapenzi basi ambaye alikua anapenda huumia kwani yeye anakua amempoeza mpenzi wake.
(2) Kushindwa Kuvumiliana; Kila mwanadamu ana tabia zake, ana mambo yake ambayo ni yake, katika mahusiano ili kuweza kudumu nilazima kila mmoja kujifunza kuvumilia na kuishi na mapungufu ya mwenzake, inapotokea mmoja kazidi au mwenzake tu kashindwa kumvumilia basi ndiyo huja kuachana.
Kuna wakati mmoja huchoka, labda kaongea sana lakini mwenzake haelewi wala hasikii basi yule anayependa huuamua kuondoka na kuacha kabisa kuvumilia.
Tyuchukulie mfano tabia kama ulevi, kupiga, umalaya, ubahili, manyanyasao na  nyingine kama hizo. Kama mwenza akichoka kuvumilia hata kama anapenda vipi, kama akiamua kujichagua yeye basi humuacha mwenzake hata kama anampenda bado na huo ndiyo hua miwisho wa uhusianao.
(3) Ameingia Mtu Mpya; Mapenzi ni ya watu wawili, anapoingia mtu mwingine wa tatu na kutaka kuingilia mapenzi basi unaweza kua mwanzo wa kuvunjika kwa mapenzi husika. Hapa mnielewe, anaweza kua ni mpenzi mpya, rafiki, ndugu hata mzazi.
Kwamba mwanaume amepata mwanamke mwingine hivyo mwanamke havumilii tena au mwanamke kapata mwanuame mwingine na mwanaume akashindwa kuvumilia. Lakini inawezekana kuna ndugu wanaingilia, wanafanya mamauzi ya mapenzi yenu.
Kuna mambo ya nnje ambayo yanaaamua aina ya maisha ambayo mnatakiwa kuishi. Yote haya yanaweza kumfanya mmoja kuchoka, kutokuona raha ya mapenzi na mwisho wa siku mnajikuta mnaachana hata kama nyie wawili mlikua mnapendana.
(4) Kuzoeana; Hii ni sababu kubwa sana ambayo huweza kuwafanya watu ambao bado wanapendana sana kuachana. Raha ya mapenzi ni upya wake, kwamba katika mapenzi hakuna kuzoeana.
Lakini wapenzi wanapoishi pamoja kwa muda mrefu, wanapokua na mahusiano ya muda mrefu, hujikuta wanazoeana, hujikuta waananza kuchukuliana poa, hapo ndiyo huanza kutokufurahia mapenzi yenyewe, huanza kukwepana na kuchokana.
Mwisho wanajikuta hawana furaha, wanajikuta hawafanyi mambo kwa pamoja kama wapenzi na kujikuta wakiachana. Kuzoeana ni tatizo, ni kitu ambacho kinaua mapenzi ya watu wnegi kwa kila mmoja kujiona kama hatendewi haki na mwenza wake kumbe wote wanafanyiana hivyo.
Nimalize makala hii kwa kukukaribisha kusoma makala nyingine kuhusu kuachana. Hapa nimezungumzia kwa ujumla sana, lakini unajua ni kwanini wanawake wengi huchwa au ni kwanini wanaume nao huchwa.

Unataka kujua nini cha kufanya baada ya kuchika, lakini unataka kujua ni namna gani unaweza kuachika na bado ukawa na furaha. Lakini je unazijua dalili za kua mwenza wako anakaribia kukucha? Basi usiumize kichwa majibu ya yote haya yatapatikana katika jarida hili hili.
Kwanini Watu Huachana Katika Mapenzi? Kwanini Watu Huachana Katika Mapenzi? Reviewed by Siabi World on July 16, 2019 Rating: 5

No comments:

title-header