Mshindi wa tuzo ya Best International Act kwenyeBET mwaka 2019 Burna Boy ametangaza tarehe rasmi ya kuidondosha Album yake ya ‘African Giant’ ambapo amesema kuwa Album hiyo itaachiwa rasmi July 26,2019.
Burna Boy ametangaza ujio wa album yake hiyo mpya “African Giant” kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo pia ametuonyesha cover ya Album ikiwa imeelezwa kuwa African Giant itabeba jumla ya ngoma 16 ikiwa tayari ngoma nne ameshaziachia ikiwemo On The Low, Dangote, Gbona na Anybody.
Album hiyo itakua ni ya nne ambapo album yake yake ya tatu ‘Outside” aliiachia January 26, 2018 ikiwa album hiyo ilijuisha midundo ya Afro Pop, Rap pamoja na dancehall ilihusisha sauti za wakali kutokea Uingereza kama J Hus, Lilly Allen and Mabel
BURNA BOY ATANGAZA RASMI TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE.....
Reviewed by Siabi World
on
July 11, 2019
Rating:
Reviewed by Siabi World
on
July 11, 2019
Rating:


No comments: